Maombi ya kuombea taifa

Shalom.tunakukaribisha uweze kushiriki pamoja nasi kuombea taifa letu na Esraeli. inawezekana wajiuliza kwa nini tuombee nchi yetu, hill swali zuri nami nimekuwekea sababu moja wapo chini japo zipo nyingi.

Kuepuka adhabu ya Mungu

Jua hili ya kwamba ikiwa viongozi au kiongozi au taifa kwa ujula litafanya uovu,Mungu huleta adhabu juu ya taifa hilo. Nimelijua hili niliposoma mstari huu
"Basi BWANA akawaletea Israeli tauni tangu asubuhi hata wakati ulioamriwa; nao wakafa watu toka Dani mpaka Beer-sheba sabini elfu."(2 Samweli 24:15). Watu hawa walikufa kwa sababu Daudi alitenda kosa na matokeo yake madhara yake ni  raia kuangamia .Naamini pangekuwepo na waombaji ili Daudi asifanye kosa au kusihi Rehema za Mungu juu ya taifa yawezekana wale watu wangeishi wasingeangamia. je wajua makosa anayo fanya Daudi wako yana adhiri namna gani taifa? Ukisoma katika maandiko utaona ya kuwa Esraeli kama taifa walipokuwa wakosa Mungua aliwadhibu kwa kuwatanya katika matifa wakawe watuma au alileta uongozi mbaya utakao kuwa mwiba kwa waesraeli.

Tunapo liombea taifa letu noi vema kukumbuka kupmba baraka juu ya taifa takatifu Esrael kwa  kuwa kuna ihusiano mkubwa wa taifa letu na maisha yetu binafsi kubarikiwa na Mungu tunapo liombea taifa la Esrael. Mungu alisema " nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa. (Mwnz 12:2)  

Haya ni maneno Mungu alimwambia Ibrahimu ambaye ndiye chimbuko la Esrael.

Kwa maneno haya machache ndugu mwombaji karibu tushirikia katika kuomba kwa ajili ya taifa letu.Tafadhali weka tutumie email yako use sehemu ya mtandao wa maombi haya