Shukrani kwako mpendwa wetu kutembelea ukrasa huu ili upate kuusoma au kutushirikisha mahitaji yako ya maombi kwa Mungu baba wa Bwana wetu Yesu kristo.
Katika maisha yapo mambo mengi sana yaletayo maumivu eitha katika mili yetu au ndani ya roho zetu.Mambo hayo yamegeuka ni mizigo mizito sana maishani mwetu. Jambo la kufurahisha ni kuwa pamoja na uwepo wa mizigo hiyo bado tunaweza kupumzika, kwani Yesu ametoa wito kwetu tumtwike yeye mizigo yetu ili sisi tupumzike "njoni kwangu wenye... kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha"(Mth:11:28)
Tunajua kuwa si rahisi kutuma ujumbe wa kutia moyo kwa kila email zinazotufikia za mahitaji ya maombi,lakini lililo mhimu ni kuwa tutaomba kwa ajili ya hitaji lako na Mungu ataskia kilo chetu
Tungependa ujue hili ya kuwa kwa kututumia mahitaji ya kukuombea unakubali kuunganisha imani yako pamoja nasi katika ulimwengu wa roho hivyo si kwamba unatuandikia sisi bali Mungu aliye pamoja nawe hata muda unapoandika na kwamba tayari amekusikia ,kumbuka Imani yako ni jicho la kukusaidia kuona mjiza wako ukikujia waziwazi ( Ebrania 11:1 ) na jambo lingine dumu ukimshukuru Mungu kwa kujibu naombi yako (wathesalonike 5:18)
Mhimu
Inawezekana ukapata jibu si sawa na vile ulihitaji,hii haimanishi kwamba Mungu hajajibu maombi yako hapana Bali kwa wema na hekima zake anaweza kukupa kile aonacho ni bora zaidi kuliko uliomba sawasawa na makusudi yake, tunajua hili kwa kuwa yeye anakuwazia mema na si mabaya hivyo tegemea kuwa anakupa kilicho chema ( Yer 29:11 )
Baada ya kutuma maombi yako ni wakati wa kurusu mapenzi ya Mungu kutimizwa na kuweka pembeni mapenzi yako na matamanio yako,tunakushauri hivi kwa kuwa tunajua Mungu huliangalia neno lake alitimize ( Her 1:12).Hii ndiyo sababu Yesu mwenyewe aliomba akisema "si kama mimi nipendayo...(Math 26:39) na ubaki katika upendo wake.
Mwisho nisema kama bado uhusiano wako na Mungu mzuri au bado hujaokoka fanya uamuzi wa kumpokea Yesu leo,uamuzi wa namna hii humpa nafasi nzuri sana kisheria sawa na sheria za ulimwengu wa roho Yesu kuwa upande wako na kukusaidia.kufuatana (warumi 8:2) kiroho mtu aweza kuwa chini ya sheria ya uzima au chini ya sheria ya mauti.unapokuwa chini ya sheria ya mauti milango inakuwa wazi kwa Shetani kukutawala na unapowa katika sheria ya Roho wa uzima milango iko wazi kwa Yesu kukusaidia na kutawala njia zako.
Tuma maombi yako kwa kujaza kisanduki hiki.
.