Hitaji la maombi


Kazi ya kujenga ufalme wa Mungu si nyepesi kabisa, hii ni kwa sababu huwa inakabiliwa na upinzani mkubwa katika ulimwengu wa roho na kimwili pia. Kazi hii huwa rahisi pale tu Mungu ambaye ndiye mfalme anaposhiriki katika ujenzi wa ufalme wake,na njia pekee ya kumshirikisha Mungu katika kazi hii mhimu ili ni kupiga magoti na kumsihi anyoshe mkono wake  na awawezeshe watumishi wake kusimama kwa uaminifu katika kazi  (Zab:127:1).

Kama huduma runa uhitaji mkubwa sana wa jeshi la waombaji watakao simama imara kwa uaminifu wakimwinulia Mungu mikono yao kwa unyeyekevu mkubwa kusihi Mungu aongozane na huduma hii kila mahali na kulidhibitisha neno lake na ufalme wake maana pasipo Yesu sisi hatufai kitu kabisa. ( Yohana 15:5).

Ukurasa huu wa maombi umegawanyika katika maeneo makubwa matatu:-

1. Maombi kwa wahitaji.
Huduma hufanya maombi kwa ajili ya watu wenye shida na m- ahitaji mbalimbali ya kimwili na kiroho - kama vile magonjwa, kazi, kuoa au kuolewa. Ikiwa utahitaji huduma hii ingia hapa

2. Maombi kwa ajili watumishi - Ikiwa wewe ni mwombaji na unapata msukumo wa kuombea watumishi na huduma hii tunakushi usisite kuungana nasi katika kuombea kutuo.bea sisi na huduma yenyewe kwani Mungu ana taka ushiriki pamoja nasi katika huduma hii kwa njia ya maombi.ingia hapa 

3. Maombi ya Taifa na Esraeli - Kama ndani yako una mzigo wa
kuombea nchi hii ya Tanzania au Esraeli, basi ungana nasi katika maombi haya kwa kingia hapa



Karibu tujenge ufalme